TATIZO LA VIDONDA VYA TUMBO
makundi makuu matatu ya vidonda vya tumbo ambayo ni; vidonda vinavyotokea kwenye mfuko wa kuhifadhia chakula, yaani tumbo (gastric ulcers), vidonda vinavyotokea kwenye sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo (duodenal ulcers) na vidonda vinavyotokea kwenye koo (oesophageal ulcers).
Hata hivyo, wataalamu wanabainisha kuwa kuna aina kuu mbili tu zinazoathiri watu wengi duniani za ugonjwa huo. Hizi ni ile inayoathiri tumbo la kuhifadhi chakula (gastric ulcers) na ya pili ni ile inayoathiri utumbo mwembamba ujulikanao kama ‘duodenam’ ambao kwa kitaalamu hujulikana kama duodenal ulcers ambapo aina zote mbili kwa ujumla huitwa peptic ulcers.
Sababu za vidonda vya tumbo
Zipo sababu kadhaa za vidonda vya tumbo la chakula na utumbo mwembamba. Hapo zamani kulikuwa na dhana kwamba msongo wa mawazo (stress) na mlo (diet) husababisha vidonda vya tumbo.
Hata hivyo, baadaye watafiti wa masuala ya afya ya binadamu waligundua kuwa tindikali izalishwayo tumboni na vimeng’enya vya pepsini inachangia kiwango kikubwa katika kusababisha vidonda vya tumbo.
Lakini hivi karibuni utafiti umeonyesha kwamba zaidi ya asilimia themanini ya vidonda vya tumbo hutokana na bakteria aitwaye heliocobacter pylori (H.pylori). Aina hii ya vimelea vya bakteria husababisha karibu asilimia 60 ya vidonda vinavyotokea kwenye tumbo (gastric ulcers) na zaidi ya asilimia 90 ya vidonda vya utumbo mwembamba (duodenal ulcers).
Vimelea vya H.pylori huweza kuishi kwenye ute ulindao tabaka la juu la tumbo na utumbo mpana. Hapo hutengeneza kimeng’enya kiitwacho urease ambacho hupunguza makali ya tindikali izalishwayo na tumbo, yaani gastric juice/acid. Ili kukabiliana na hali hii, tumbo hutengeneza tindikali nyingi zaidi ambayo huathiri tabaka la juu la utumbo.
Vimelea hivi pia hudhoofisha ute ulindao tabaka la juu la utumbo, hivyo kushindwa kulinda tumbo na utumbo mwembamba sawasawa.
Vimelea vya Hpylori huweza kusambaa kupitia chakula na maji. Vimelea vya bakteria hawa pia hupatikana kwenye mate, hivyo vyaweza kuambukizwa kupitia kinywa haswa iwapo mtu atabusiana na muathirika wa vimelea hivyo. Watu wengi pia huathirika na vimelea hivi utotoni.
Wataalamu wanabainisha kuwa matumizi ya dawa kwa muda mrefu ni moja ya sababu ya vidonda vya tumbo. Hii ufanya ukuta wa utumbo kujilinda na madhara yatokanayo na tindikali ya utumbo kwa kuwa na utando laini ambao hutolewa na vichocheo vijulikavyo kama prostaglandins.
Dawa huharibu mfumo wa kutengeneza vichocheo prostaglandins na hivyo kufanya kuta za tumbo kukosa utando wa kuzilinda na mashambulizi ya tindikali hali ambayo husababisha kutokea kwa vidonda vya tumbo.
Uvutaji wa sigara: Kafeini na nicotine ambayo hupatikana kwenye baadhi ya vinywaji kama soda, kahawa pia kwenye sigara huchangamsha utengenezaji wa tindikali ya gastric tumboni ambayo huchubua ukuta wa utumbo na pia hutonesha kidonda kilichopo kama mtu ni mwathirika.
Ingawa inasadikika kwamba vigezo vyote hapo juu huchangia kupata vidonda vya tumbo, bakteria hpylori anasadikiwa kuwa chanzo kikuu katika kusababisha vidonda vya tumbo.
Aidha, wataalamu wanasema kuwa sababu za kijenetiki/vinasaba navyo ni moja ya kupata tatizo hilo la vidonda vya tumbo.
Historia ya kuwepo kwa vidonda vya tumbo katika ukoo au familia yaweza kuchangia ndugu wa ukoo au familia husika kupata vidonda vya tumbo. Pia, tafiti zimeonyesha uhusiano kati ya watu wenye kundi la damu la O na uwezekano wa kupata vidonda vya tumbo.
Vidonda vya tumbo/mfuko wa chakula (gastric ulcers) na dalili zake
Waathirika wa aina hii ya vidonda vya tumbo huwa wembamba kutokana na kutokula wakihofia kupata maumivu pindi walapo chochote.
Dalili kubwa ya wagonjwa hawa ni; maumivu makali au kiungulia maeneo ya chembe moyo (epigastic pains), maumivu juu kidogo ya tumbo ambayo mara nyingi huendana na muda wa kula chakula.
Mtu mwenye vidonda kwenye tumbo hupata maumivu makali sana kipindi anapokula au mara tu baada ya kumaliza kula wakati aliye na vidonda kwenye sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo (duodenal ulcers) hupata maumivu makali anapokuwa na njaa na hupata nafuu pindi anapokula. Pia hamu ya kula kupungua na baadhi yao waweza hata kutapika.
Pia kutapika damu (haematemesis) na kupata choo chenye damu (malaena) huweza kuambatana na aina hii ya vidonda vya tumbo. Uzito wa mwili hupungua kwa kiasi fulani kutokana na kutokula vizuri. Kusambaa kwa maumivu hadi mgongoni kwaweza kutokea iwapo kidonda kimetoboka na kuhusisha kongosho (pancreas).
Dalili za utumbo mwembamba (duodenal ulcers)
Maumivu yana tofauti na aina ya kwanza. Mara zote maumivu ya vidonda katika utumbo mwembamba hutokea kwa kipindi cha kati ya saa mbili na nusu hadi nne baada ya mlo ambapo chakula huwa kimeisha tumboni (hunger pains).
Maumivu pia hutokea zaidi mapema asubuhi au nyakati za jioni. Nafuu hupatikana kwa kula chakula. Kutapika hutokea kwa nadra sana japo kutapika damu na kupata choo chenye damu hutokea mara nyingi zaidi kuliko aina ya kwanza.
Hamu ya kula kwa wagonjwa wa aina hii huwa nzuri na hupenda kula mara kwa mara, hivyo huwa na miili yenye afya nzuri tofauti na wagonjwa wa aina ya kwanza.
Kuvimbiwa au tumbo kujaa gesi
Hali hii pia yaweza kuendana na kubeua au kujamba mara kwa mara hali ambayo hufunga choo na kufanya chakula kukaa muda mrefu katika utumbo na kusababisha maozea ambayo huleta maambukizi ya bakteria. Pia kuongezeka kwa mate yanayoshuka tumboni baada ya kucheua hali ambayo huleta kichefuchefu.
Uwepo wa dalili kama kiungulia cha muda mrefu, kucheua, kutapika baada ya kula na zingine nyingi nilizozitaja ni ishara tosha ya kumfanya mhusika kumuona daktari ili amfanyie uchunguzi ili kujiridhisha kuwa hana tatizo la vidonda vya tumbo au analo.
Pia ni muhimu kuzingatia dozi kwa kunywa dawa katika muda uliopangwa na kumaliza dozi hata baada ya dalili (maumivu) kupotea. Ugonjwa wa vidonda vya tumbo tofauti na inavyodhaniwa waweza kupona kabisa kama magonjwa mengine.
Imeandaliwa kwa msaada wa mtaalamu Siroum Sanitarium. Mwandishi anapatikana kwa simu; 0719076376.

2 comments:
Naam Asante sana kwa muelezo wako umetambaa vizuri kabisa ila mm nimepima kipimo kiitwacho Endoscopy ndani ya south africa ikaambiwa kuwa nina Gastritis nasina vidonda hivyo nilipewa vidinge vya kutumia LANSOPRAZOL kwa muda wa miezi6 nimevitumia kwa muda wa mwezi m1 bila mafaanikio ila ilikua inaumaaa nainapoa yenyewe bila dawa nilipimwa bacteria H.Pyl nasijakutwa nazo! Sasa inaonyesha kuna maradhi mengine wachawi uwa wanampiga mtu uku wakitegezea kwenye naradhi ya kizungu sasa mkisha ona mme mpa mgonjwa dawa na hapati nafuu mnatakiwa kumueleza ukweli yende kwenye tiba Asilia niushauri tu mm nimebadilishiwa dawa mpaka kila ninapo tumia dawa ndio nazidi kua mgonjwa. Hassanmaabadi@gmail.com kwa mawasiliano zaidi

Post a Comment